DMG Yakabidhi Rasmi Kivuko cha MV Tanga Kwa Serikali

Leo 14/12/2022 Kampuni ya Dar es Salaam Merchant Group imekabidhi rasmi kivuko cha MV Tanga baada ya kukamilisha ukarabati mkubwa uliodumu kwa miezi 4.

Hafla ya makabidhiano ya kivuko hiko imefanyika katika wilaya ya Pangani na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa serikali, akiwamo Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Mh. Omary Mgumba, mkuu wa wilaya ya Pangani, Mh. Ghalib Lamsema na Mbunge wa Pangani, Mhe. Juma Aweso.

Mkuu wa mkoa wa Tanga Mh. Omary Mgumba alionyesha kufurahishwa na weledi na ufanisi mkubwa ulioonyeshwa na kampuni ya DMG katika kukamilishia ukarabati wa kivuko cha MV Tanga.

“Naipongeza Kampuni ya Dar es Salaam Merchant Group kwa kazi hii kwa kuifanya kwa weledi na kuikamilisha kwa wakati. Hakika wamejitangaza vyema na wameiaminisha serikali kuwa Watanzania tukipewa fursa tunaweza.” Alisema Mh. Omary.

Mtendaji mkuu wa Dar es Salaam Merchant Group, Rayton Kwembe alitoa shukrani zake kwa serikali kwa kuwaamini na kuwapa kipaumbele wakandarasi wa ndani katika kutekeleza miradi ya maendeleo na kuahidi kutumia fursa hizi kwa weledi.

“Tunaishukuru serikali inayoongozwa na Mh. Dr. Samia Suluhu Hassan kwa kutuamini wakandarasi wa ndani. Tunaahidi kuendelea kufanya kazi hizi kwa weledi na ubora wa kimataifa na kuwa sehemu ya maendeleo muhimu ya serikali na nchi yetu.” Alisema Rayton.

Kivuko cha MV Tanga kilikuwa kinafanyiwa ukarabati kwa muda wa miezi minne. Ukarabati huu ulihusisha  maeneo tofauti ya Kivuko kama vile maeneo ya abiria na maegesho ya magari, uvungu wa kivuko, milango ya kivuko na chumba cha kuongozea kivuko hiko. Kivuko hicho kina uwezo wa kubeba abiria 100 na magari madogo 6.

Makabidhiano haya yanakifanya kivuko cha MV Tanga kuendelea na kazi yake hivyo kuwa sehemu muhimu ya maendeleo ya miundombinu na biashara mkoani Tanga.

“Kiukweli tunajisikia kama tumependelewa, hasa sisi wafanyabiashara. Tulikuwa tunatumia fedha nyingi kuvuka kwenda Mbweni na kurudi. Na wakati mwingine kuhatarisha maisha kwani tulikua tunavuka kwa kutumia mitumbwi na boti ndogo. Kivuko cha MV Tanga ni msaada mkubwa sana kwetu.” Alisema Bi. Fatma Ndosi, mfanyabishara mdogo wilaya ya Pangani.

1 thought on “<strong>DMG Yakabidhi Rasmi Kivuko cha MV Tanga Kwa Serikali</strong>”

  1. Wonderfully job my dream company
    Sorry am a student pursuing bachelor degree in naval architecture and marine engineering
    Can I apply for field training?
    kindly 0772347435

    Reply

Leave a Comment